Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, June 21, 2017

YANGA YASALIMU AMRI KWA NIYONZIMA, YATANGAZA KUACHANA NAYE RASMI



 Image result
Yanga imeamua kuachana na kiungo mshambuliaji wake, Haruna Niyonzima baada ya kutofikia makubaliano ya mkataba mpya.
Katibu wa Yanga  Charles Mkwasa amesema wanaachana na Niyonzima vizuri tu baada ya mazungumzo baina yao kutofikia mwafaka wa mkataba mpya.
“Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia muafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia ya kuendelea naye kwa misimu miwili ijayo,”alisema.
Juzi Niyonzima alisema yuko kwenye mazungumzo na Yanga juu ya mkataba mpya na wakati huo huo Simba nao wanamuhitaji.
Tangu jana kumekuwa na taarifa za Haruna kusaini Simba, ingawa yeye mwenyewe kila anapotafuta amekuwa hapatikani kwenye simu yake.
Niyonzima alijiunga na Yanga mwaka 2011, akitokea APR ya Rwanda aliyoanza kuichezea mwaka 2007 baada ya kujiunga nayo kutoka Rayon Sport iliyomsajili mwaka 2006 kutoka Etincelles iliyomuibua kisoka nchini humo.

No comments:

Post a Comment