Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 19, 2017

MECHI ZOTE ZA MWISHO VPL KUANZA SAA 10.00 JIONI.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tunafahamisha kuwa mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017zitachezwa kuanzia saa 10.00 jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama.
Muda huo umepangwa ili kuhakikisha timu zote zinamaliza mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinamalizika siku moja ya Mei 20, mwaka huu na kwa muda mmoja, ikiwa ni pamoja na kudhibiti viashiria vyo vyote vya upangaji wa matokeo.

Ni jukumu la kila kamishna kuhakikisha mechi anayosimamia inaanza katika muda ulipangwa bila kujali kama kuna mgeni rasmi au la.