Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 22, 2017

MALINZI AMALIZA UTATA WA NANI MFUNGAJI BORA 2016/2017
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi ameondoa utata na  mabishano ya mashabiki wa soka nchini juu ya nani atapata zawadi ya mfungaji bora baada ya wachezaji wawili kufungana kwa idadi sawa ya mabao.
Wachezaji hao ni Simon Msuva wa Yanga na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, ambao kila mmoja amefanikiwa kutupia mabao 14.
Kwa mujibu wa Tweet ya Malinzi aliyotoa  leo, wachezaji wote kwa kuwa wamelingana idadi ya mabao,  hivyo watapewa zawadi sawa.
“Kwa kuwa vijana wetu Mussa na Msuva wamefunga mabao 14 wote ni wafungaji bora na watapewa zawadi sawa sh. Milioni 5.8,”alisema.
Mbali na wachezaji hao wanaowania tuzo ya mfungaji bora,  kutakuwa na tuzo nyingine ikiwemo kikosi bora cha msimu, tuzo ya mchezaji bora mwenye umri chini ya miaka 20, tuzo za bingwa wa Ligi Kuu, mshindi wa pili, wa tatu na nne.
Sherehe za utoaji tuzo zinatarajiwa kutolewa Mei 24, mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Wafuatao wameteuliwa kuwania tuzo hizo kutokana na vigezo mbalimbali:
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu: Aishi Manula – Azam, Simon Msuva – Yanga, Shiza Kichuya – Simba, Haruna Niyonzima– Yanga, Mohammed Huseein -Simba
Kipa bora: Aishi Manula– Azam, Owen Chaima – Mbeya City, Juma Kaseja – Kagera Sugar.
Kocha Bora: Joseph Omog – Simba, Mecky Maxime – Kagera Sugar, Ettiene Ndayiragije – Mbao.
Mmwamuzi bora : Shomari Lawi – Kigoma, Elly Sasii – Dar es Salaam, Hance Mabena – Tanga
Mchezaji bora wa kigeni: Haruna Nyonzima – Yanga, Method Mwanjale – Simba, Yusuph Ndikumana – Mbao
Mchezaji bora  anayechipukia : Mbaraka Abeid – Kagera Sugar, Shaaban Idd – Azam, Mohammed Issa – Mtibwa.
Tuzo ya Ismail Khalifan  (U-20): Shaaban Idd – Azam, Abdalah Masoud – Azam, Mosses Kitambi – Simba.
Tuzo ya heshima: (Atatangazwa aliyeteuliwa siku hiyohiyo ya sherehe za tuzo), goli bora la msimu: (Tayari yamepatikana mabao bora 10 ambayo yataoneshwa siku hiyo ukumbini ikiwemo lile bora la msimu mzima) na timu yenye nidhamu (Mshindi atatangazwa ukumbini).