Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

JONAS MKUDE ATEMWA TAIFA STARS



Image result
NAHODHA Msaidizi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Jonas Mkude ameenguliwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kitachoondoka kesho kwenda Misri kwa kambi ya wiki moja.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema kwamba Mkude hatakuwako kwenye msafara huo kutokana na ushauri wa madaktari walioelekeza mchezaji huyo apate mapumziko ya angalau siku nne kuweka akili sawa baada ya ajali aliyopata jana.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ameridhia na kusema kuwa Mkude ataungana na wenzake Juni 8, mwaka huu timu itakaporejea kutoka Misri.
Mkude na watu wengine akiwemo dereva, walikuwa kwenye Totota Land Cruiser V8 iliyopinduka eneo la Dumila kufuatia gurudumu kupasuka.
Mtu mmoja Shose Fidelis alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro, wakati wengine, Jasmin na Faudhia wamelazwa hospitalini hapo na dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanaye kwa jina la utani, Rais wa Kibamba anashikiliwa na polisi.
Mkude alikuwa anatoka Dodoma, ambako juzi aliisaidia Simba kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti, kinatarajiwa kuondoka kesho Jumanne saa 10.45 jioni kwenda Misri.
Taifa Stars ambayo itakuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kesho saa 7. 45 mchana inakwenda Misri kufanya kambi ya siku nane kujindaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaochezwa Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment