SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika limepitisha majina 21 ya
wachezaji kwa Timu za Vijana ya Taifa waliochini ya miaka 17 ambayo zinashiriki
Fainali za 12 Afika zinazotarajiwa kuanza Mei 14-28 nchini Gabon.
Katika taarifa iliyowekwa cafonline imetoa orodha ya wachezaji
wa timu zote nane ambazo zinashiriki fainali hizo.
Pia taarifa hiyo inasema
timu zitakazofuzu nusu fainali zitakuwa zimefuzu kuwakilisha
Afrika katika fainali za FIFA U-17 zitakazofanyika nchini India kuanzia Oktoba
06-28 2017.
Katika orodha ya wachezaji
waliopitishwa jina la mchezaji, jina la jezi, nafasi anayocheza, mwaka
aliozaliwa na timu anayochezea.
Wakati nchi
zingine zinaonyesha timu ambazo wachezaji wao wanachezea ama wanatoka,
wachezaji wa Tanzania wanaonekana hawana timu wanazochezea.
Kikosi
cha Serengeti boys kilichopitishwa ni Ramadhan
Kabwili, Ally Ng’anzi, Nickson Kibabage, Enrick Vitalis, Dickson Job, Issa
Makamba, Cyprian Benedictor, Saidi Mussa na Abdul Suleiman
Wengine
ni Assad Juma, Mohamed Rashid, Kibwana Ally, Shaaban Ada, Ally Msengi, Yohana
Mkomola, Israel Mwenda, Ibrahim Abdallah, Samwel Edward, Muhsin Malima, Kelvin
Kayego na Kelvin Nashon.
GONGA JINA LA NCHI KUTAZAMA KIKOSI CHAKE
Kundi A
Ghana
Kundi B
Kundi B
No comments:
Post a Comment