Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 3, 2017

LIPULI KUPANDA LIGI KUU KESHO?LIGI Daraja la kwanza inatarajiwa kuendelea kesho kwenye viwanja tisa tofauti, huku Lipuli ikitarajiwa kutangaza kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Akizungumza na gazeti hili, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema timu 18 zinatarajiwa kushuka uwanjani katika miji tisa tofauti.
Vinara wa Kundi A Lipuli ambao wanatafuta pointi moja kujihakikishia kupanda ligi kuu msimu ujao itaialika Polisi Dar, Kiluvya itacheza na Pamba, Friends Ranger itakuwa mwenyeji wa African Sports mchezo utakaochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B Polisi Moro itakuwa mwenyeji wa KMC kwenye Uwanja wa Jamhuri,mchezo ambao utaamua nani awe juu ya mwenzake kwani wote wana pointi 19.
Coastal Union itaialika Mlale JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, Mbeya Warriors itacheza na vinara wa kundi B Njombe Mji yenye pointi 21.
Kundi C Polisi Mara itacheza na vinara Singida Utd yenye pointi 26, Mvuvumwa itacheza na Alliance yenye pointi 23 kwenye nafasi ya pili na Rhino Rangers ambayo inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 21 itacheza na Polisi Dodoma.
 Jumapili Mgambo Shooting itacheza na Panone kwenye Uwanja wa Mkwakwani na  Ashanti itacheza na Mshikamano kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.