Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, February 3, 2017

BREAKING NEWSSSSSS!!!!! SERENGETI BOYS ILEEE FAINALI ZA VIJANA AFRIKA

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) limeirejesha Tanzania kushiriki katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kushinda rufaa yake.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimkatia rufaa mchezaji wa Congo Brazzaville, Langa-Lesse Bercy aliyechezeshwa baada ya kuzidi umri.
Katika mchezo wa mwisho kabla ya kufuzu, Serengeti Boys ilishinda bao 3-2 jijini Dar es Salaam kabla ya kufungwa 1-0 na kutolewa kwa faida ya bao la ugenini.
TFF ilikata rufaa kupiga kuchezeshwa kwa mchezo huyo, ambapo Caf iliamuru afanyiwe vipimo vya kugundua umri wake halisi,  lakini mara kadhaa mchezaji huyo hakutokea.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye jioni hii alikaririwa na Radio ya TBC Taifa, ambapo alithibitisha kuwa, Tanzania imeshinda rufaa yake na sasa itashiriki fainali hizo za Mataifa ya Afrika kwa vijana yatakayofanyika baadae mwaka huu.
Serengeti Boys inaendelea na maandalizi ya mashindano katika hostelini za TFF zilizopo Karume tayari kushiriki mashindano.
Tanzania iliondolewa kushiriki katika fainali za mwaka 2005 zilizofanyika Gambia baada ya kumchezesha Nurdin Bakari aliyezidi umri.