Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 3, 2017

USHINDI WA MABAO 6-0 WAMPA KIBURI MWAMBUSIKOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema katika kundi lake hakuna mechi rahisi hivyo anazichukuliwa kwa umakini mkubwa timu zote kwenye kundi leo.
Mwambusi alisema hayo wakati akizungumza waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo kwa ushindi wa 6-0 dhidi ya Jamhuri kwenye Kombe la Mapinduzi.
“Mimi kwangu kila mechi ni ngumu kwani timu zote zipo katika mashindano na nina hakika zimejiandaa, kazi kumbwa iliyopo ni kupambana,” alisema Mwambusi
Pia alisema ushindi wake wa bao nyingi ni mwanzo mzuri lakini haoni kama ni mechi rahisi kwa vile kila timu imejiandaa kimashindano.

Mwambusi alisema licha ya ushindi mkubwa dhidi ya Jamhuri, wachezaji wake walifanya kazi ya ziada kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwani walisoma mapungufu ya washindani wao na kujipanga  kwa kutumia mapungufu hayo na kupata ushindi.

Hata hivyo alisema kwamba bado anaendelea kukiweka sawa kikosi chake ili kuzidi kufanya vyema zaidi katika mechi zijazo.

Mabao ya Yanga Simon Msuva na Donald Ngoma ambao kila mmoja alifunga mawili na Thabani Kamusoko na Juma Mahadhi wakifunga bao moja kila mmoja.