Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 3, 2017

JANET BALAMA, MWANAHAMISI NA ELL SASII WAULA FIFA




TANZANIA imefanikiwa kutetea nafasi zake 18 za waamuzi wenye beji za Fifa kwa msimu wa 2017.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye www.fifa.com inasema Tanzania imefanikiwa kupata beji 18, wanawake  beji saba na wanaume 11.
Waamuzi wa kati waliopata beji kwa upande wa wanaume ni Israel Mujuni, Nassor Mfaume, Marthin Saanya, Elly Sasii ambaye amechukua nafasi ya Waziri Sheya ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
Waamuzi wasaidizi wanaume ni Josephat Bulal, Fernand Chacha, John Kanyenye, Kinduli Mgaza, Frank Komba, Soud Lila na Samwel Mpenzu.
Kwa upande wa wanawake wanaopuliza filimbi ni Florentina Zablon, Jonesia Rukyaa na Mwanahamisi Matiku ambaye amechukua nafasi ya Sophia Mtogole ambaye alishindwa kutetea beji yake.
Waamuzi wasaizi wanawake ni Grace Wamala, Dalila Jafari, Hellen Mduma na Janet Balama ambaye amechukua nafasi ya Kudra Omar ambaye alishindwa kutetea beji yake.
Kwa ukande wa Afrika Mashariki na Kati, Sudan inaongoza ikiwa na waamuzi 28 ikifuatiwa na Uganda yenye waamuzi 22, Rwanda yenye waamuzi 20 na Tanzania inashika nafasi ya nne na waamuzi 18.
Burundi na Kenya zikikabana kwenye nafasi ya tano zikiwa na waamuzi 16 kila moja, Somalia ina waamuzi tisa na Sudan Kusini ina waamuzi nane.
Brazili inaongoza kwa dunia ikiwa na waamuzi 40, ikifuatiwa na Spain yenye waamuzi 37 ikifuatiwa na Argentina yenye waamuzi 36, ujeruman waamuzi 33 na Misri inaongoza kwa bara la Afrika ikiwa na waamuzi 32.



No comments:

Post a Comment