Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 3, 2017

RAUNDI YA PILI LIGI YA WANAWAKE KUANZA KESHO





RAUNDI ya pili ya Ligi Kuu ya Wanawake inatarajia kuanza leo katika viwanja vinne kwenye miji tofauti vikiwaka moto.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema kundi B litakuwa na mechi mbili ambazo ni za Majengo FC itacheza na Marsh AFC kwenye Uwanja wa Namufua Singida.
“Ligi Kuu ya wanawake ilisimama kupisha usajili wa dirisha dogo hivyo kesho (leo) inatarajia kuanza kwenye viwanja vya miji ya Bukoba, Singida, Iringa na Dar es Salaam,” alisema Lucas
Mchezo mwingine wa kundi B ni kati ya Panama FC na Sisterz ya Kigoma utakaochezwa Uwanja wa Samora Iringa na Victoria Women ya Kagera wataialika Baobab FC kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Kundi A Mburahati FC itacheza na Viva ya Mtwara kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na kesho Evergreen itacheza na Fair Play kwenye Uwanja wa Karume na Mlandizi FC wataikarisha JKT Queens kwenye Uwanja wa Mabatini Pwani.
JKT Queens inaongoza kundi B ikiwa na pointi ikwa na 13 ikifuatiwa na Mlandizi yenye pointi kumi, Evergreen yenye pointi tisa, Mburahati yenye pointi mbili, Viva yenye pointi moja na Fair play ikiburuza mkia bila pointi.
Kundi B linaongozwa na Sisterz yenye pointi 15, ikifuatiwa na Marsh yenye pointi kumi, Panama yenye pointi nane, Baobab yenye pointi mbili na Victoria Women inaburuza mkia ikiwa na pointi moja.

No comments:

Post a Comment