Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 17, 2016

Waziri Nape afungua tamasha la michezo la Karatu 2016


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amefungua Tamasha la Michezo la Karatu lililofanyika leo
Mratibu wa tamasha hilo, ambaye ia ni mwanariadha wazamani na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Riadha Tanzania (RT), Meta Petro alisema, Waziri Nape ndiye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo, ambalo hufanyika kila mwaka.
Mbali na mbio za kilometa 10 kwa wanawake na wanaume, tamasha hilo pia limekuwa likishirikisha michezo ya mbio za baiskeli za kilometa 60, mbio za watoto za kilometa 2.5 na michezo ya mpira wa wavu na soka, ngoma za utamaduni, sarakasi pamoja na kwaya.
Kwa mujibu wa Petro, mchezo wa mpira wa wavu na soka, fainali zake zilifanyika Ijumaa Desemba 16, lakini washindi watakabidhiwa zawadi zao pamoja na wenzao wa riadha na baiskeli Jumamosi Desemba 17 siku ya kilele cha tamasha hilo, ambalo hudhaminiwa na Olympic Solidarity kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na FBF.
 Msisimko mkubwa unatarajiwa kuibuka katika mbio za kilometa 10 kwa wanawake na wanaume pamoja na zile za baiskeli, ambazo washiriki wake wengi wanatoka mjini Arusha na maeneo mengine ya Karatu, Mto wa Mbu, Manyara na kwingineko.
Mechi za soka na mpira wa wavu ambazo huanzia ngazi ya chini na kushirikisha timu kibao,  kabla ya kucheza fainali na kupata washindi wa michezo hiyo, ambao hukabidhiwa zawadi nono kutoka kwa waandaaji,
Baadhi ya zawadi zinazotolewa na Taasisi ya Filbert Bayi Foundation (FBF), ambao ndio waandaaji ni pamoja na fedha taslimu, mipira, nyavu za magoli ya mchezo wa soka, jezi, glovu na vifaa vingine.
Pia kwa upande wa mchezo wa mpira wa wavu, vifaa vinavyotolewa kwa washindi mbali na fedha taslimu ni pamoja na mipira, wavu za kuchezea na vifaa vingine vya mchezo huo, ambyo mjini Karatu huchezwa zaidi na timu za madhehebu ya kidini.
Petro alitaka wanariadha watakaoshiriki mbio hizo wajitahidi kujisajili mapema ili kujua idadi kamili ya watakaoshiriki badala ya kusubiri siku ya mwisho ndio kujitokeza,  kwani ina wapa wakati mgumu waandaaji kupanga taratibu mbalimbali.
Kwa ujumla zawadi katika michezo mbalimbali ya Tamasha la Karatu ni za kuvutia na zimeanufaisha  wanamichezo binafsi na timu kwa kupata fedha taslimu na vifaa vya michezo, ambavyo vinasaidia kuongeza ari ya kushiriki katika michezo na kuinua vipaji.

No comments:

Post a Comment