Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 13, 2016

TFF NA TAASISI YA TIBA YA MOYO YA JK KUSHIRIKIANA KUTOA MAFUNZO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeanza mazungumzo na Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyoko Muhimbili, Dar es Salaam  kwa ajili ya kushiriana kutoa mafunzo kwa madaktari na wahudumu wa afya kwa wanamichezo wa soka katika kushughulikia matatizo ya moyo.
Ni matumaini yetu kuwa mafunzo haya yataboresha uwezo wa madaktari wa mpira wa miguu sambamba na kusambazwa kwa vifaa maalumu vya tiba ya moyo kwenye klabu za soka nchini.
Hii ni hatua thabiti inayochukuliwa na uongozi wa TFF baada ya kutokea vifo vinavyosababishwa na mshtuko wa moyo kwa wachezaji ukiwamo ugonjwa wa ‘cardiac arrest’ ambao kwa taarifa za awali  unaonyesha ndio uliosababisha kifo cha Mchezaji wa Mbao FC U20, Ismail Mrisho Khalfan.
Marehemu Ismail Mrisho Khalfan alifariki dunia baada ya kuanguka uwanjani Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera wakati timu yake ya Mbao ikicheza na Mwadui katika mechi ya ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.
 Kifo hicho kimegusa hisa za wanafamilia wengi wa mpira wa miguu akiwamo Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA), Bw. Gianni Infantino ambaye juzi alituma salamu za rambirambi kwa Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Emil Malinzi kutokana na kilo cha ghafla cha Mchezaji.
Salaam Rais Infantino, zinakwenda sambamba na za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Ndugu Nape Nnauye na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou.
Mchezaji Ismail Mrisho Khalfan wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza, kilitokea Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera wakati timu yake ikicheza mchezo huo dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.
Timu hiyo ya Vijana wa Mbao, kama vilivyo timu nyingine 7 za Ligi kuu ya Vodacom, ilikuwa Kituo cha Bukoba katika Ligi ya avijana ambayo kwa msimu huu imefanyika kwa mara ya kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa kituo cha Dar es Salaam.
Ismail aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani, lakini baadaye taarifa za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.
Kamati ya Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha mchezaji huyo kabla ya baadaye kutoa taarifa za kamili ya kitatibu kujua hasa chanzo hasa cha kifo cha mchezaji huyo ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa Kagera. Marehemu Ismail Mrisho Khalfan alizikwa Desemba 5, 2016 jijini Mwanza.
…………………………………………………………………………………………………

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

No comments:

Post a Comment