SIMBA na Azam FC kesho zinashuka dimbani kusaka pointi tatu kwenye viwanja tofauti katika michezo yao ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba itakuwa mgeni kwenye uwanja wa Nangwanda
Sijaona Mtwara dhidi ya Ndanda FC na Azam
FC ikikaribishwa na African Lyon kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Wekundu hao wa Msimbazi huenda wakaendeleza rekodi
yao ya kuifunga Ndanda FC baada ya
mchezo wao wa mzunguko wa kwanza kuwachapa mabao 3-1 katika mechi iliyochezwa
Dar es Salaam.
Mchezo huo utakuwa wa kwanza katika ligi kwa kipa
mpya wa Simba Mghana Daniel Agyei ambaye anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha
kwanza baada ya kipa Vicent Angban wa
Ivory Coast kusitishiwa mkataba wake.
Pia, wachezaji wengine wapya ni kiungo James Kotei,
mshambuliaji Pastory Athanas, Juma Luizio, Moses Kitandu na beki Vicent Costa.
Simba yenye pointi 35 inahitaji ushindi katika mchezo huo ili
kurejea kileleni mwa msimamo baada ya jana Yanga kuishusha. Yanga inaongoza kwa
pointi 36 sasa.
Vile vile, Ndanda FC
yenye pointi 19 iliahidi kufuta rekodi ya kufungwa na timu hiyo
ikijivunia kusajili wachezaji wawili wapya Ayub Shaban na Ismail Mussa
watakaokuongeza nguvu.
Kwa upande wa Azam FC yenye pointi 25 itacheza leo kwenye uwanja wa Uhuru ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya
bao 1-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa
Chamazi.
Pengine, mchezo wa leo Azam FC kwa vile imefanya
mabadiliko makubwa ikafanya vizuri tofauti na African Lyon yenye pointi 17 ambayo imeondokewa na wachezaji wake wengi
waliojiunga na Mbeya City.
Wachezaji wapya wanaotarajiwa kuwemo kwenye kikosi
cha Azam FC ni Samwel Afful, Mohamed Yahaya, Yakubu Mohamed, Enock Agyei,
Stephani Kingue, Joseph Mahundi na Abdallah Kheri.
Azam FC inahitaji kushinda katika mchezo huo ili
kuingia katika mbio za kuligombania taji la ligi.
Pia, Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji kwenye uwanja
wa Sokoine jijini Mbeya dhidi ya Majimaji huku Mbao FC ikiwa kwenye uwanja wa
CCM, Kirumba Mwanza ikiwakaribisha Stand United.
No comments:
Post a Comment