Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 17, 2016

MSUVA AFUNGA MABAO MAWILI YANGA IKIISHUSHA SIMBA KILELENIYANGA imerudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu bara baada ya kuifunga Ruvu Shooting mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Ikicheza chini ya kocha wake mpya Mzambia George Lwandamina, Yanga ilitawala vipindi vyote vya mchezo huo na kutoa burudani safi kwa mashabiki wake waliofika uwanjani hapo.
Yanga iliandika bao la kuongoza katika dakika ya 38 baada ya mchezaji wa Ruvu kujifunga akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Simon Msuva.
Dakika ya 57, msuva aliandika bao la pili baada ya kuunganisha pasi ya Deus Kaseke kabla ya kuongeza bao la tatu katika dakika ya 90 baada ya kuunganisha pasi ya Haruna Niyonzima.
Mechi ilikuwa ya upande mmoja zaidi kwa Yanga kufanya mashambulizi langoni mwa Ruvu mara kwa mara ambapo katika dakika ya 52 nusura Amisi Tambwe aandike bao baada ya kuachia shuti kali lililopanguliwa na Hamisi Seif.
Dakika mbili baadae kocha Lwandamina anafanya mabadiliko kwa kumtoa Tambwe na nafasi yake kuchukuliwa na Said Makapu.
Dakika ya 59 Ally Bilal alifanya shambulizi la nguvu na nusura aipatia Ruvu bao lakini kutokuwa makini kulimfanya kupiga shuti dhaifu lililodakwa na kipa wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’.
Kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mwadui ilishinda bao 1-0 dhidi ya Toto Africans na kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya wenyeji Mbeya City walilazimishwa suluhu na Kagera huku Ruvu Shooting wakitoka sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi.