Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 26, 2016

LIGI KUU LEO MABATINI, JUMATANO YANGA DHIDI YA NDANDA, MTIBWA vs MAJIMAJI


VPL, Ligi Kuu Vodacom, inaendelea Leo kwa Mechi moja huko Mabatini, Mlandizi ambako Ruvu Shooting watacheza na Tanzania Prisons.
Mechi hii inazikutanisha Prisons ambayo ipo Nafasi ya 7 ikiwa na Pointi 22 na Ruvu Shooting ikiwa Nafasi ya 9 na ina Pointi 20.
VPL itaendelea tena Jumatano Desemba 28 kwa Mechi 2 ambako huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Mabingwa Watetezi Yanga kucheza na Ndanda FC na huko Manungu, Morogoro, Mtibwa Sugar watacheza na Majimaji FC.

Alhamisi pia zipo Mechi 2 kati ya Ruvu Shooting na Simba na nyingine ni Azam FC dhidi ya Tanzania Prisons.

Hadi sasa, Simba wapo kileleni wakiwa na Pointi 41, Yanga ni wa Pili wenye Pointi 37 na Kagera Sugar wanakamata Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 28,Azam Fc wanafuatia wakiwa na Pointi 27 sawa na Mtibwa Sugar.

VPL
Ligi Kuu Vodacom
Jumatatu Desemba 26

Ruvu Shooting v Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandazi]

Jumatano Desemba 28

Yanga v Ndanda FC [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Majimaji FC [Manungu, Manungu]

Alhamisi Desemba 29

Ruvu Shooting v Simba [Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam]
Azam FC v Tanzania Prisons [Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam]

Jumamosi Desemba 31

Mwadui FC v Kagera Sugar [Mwadui Complex, Mwadui]
African Lyon v JKT Ruvu [Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam]
Mbeya City v Mbao FC [Sokoine, Mbeya]

Jumapili Januari 1
Toto African v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]