Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 5, 2016

LIGI YA VIJANA U-20 KUANZA NOVEMBA 15 KWENYE KITUO CHA BUKOBA NA DAR ES SALAAMLIGI ya Vijana ya Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) wenye umri wa chini ya miaka 20, inatarajiwa kuanza Novemba 15, 2016 mwaka huu kwa kushirikisha timu za vijana U-20 wa timu za ligi kuu.
Uzinduzi utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera kwa timu za vijana za Kagera Sugar na Yanga kuchuana siku hiyo.
Akizungumza na wandishi wa habari, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema timu zimepangwa kwenye makundi mawili yenye timu nane kila moja.
"Kagera na Yanga zimepangwa kundi A na zitaanza mchezo saa 10.30 jioni ikiwa ni baada ya shamrashamra za uzinduzi wake kwani kulingana na ratiba iliyotolewa na bodi ya Ligi siku hiyo kutakuwepo na mechi moja lakini kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi ya TFF kwa siku kutakuwa na michezo miwili kwa tofauti ya saa", alisema Lucas 
Timu nyingine ambazo zipo kundi A ni Stand United na Mwadui za Shinyanga ambazo zitacheza Novemba 16, 2017 na Novemba 17, Azam itacheza na Mbao FC saa 8.00 mchana kabla kuzipisha Toto Africans na African Lyon saa 10.30 jioni.
Kundi B kituo chake kitakuwa Dar es Salaam, Simba itafungua dimba na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Uhuru - mchezo utakaonza saa 8.00 kabla ya kuzipisha timu za JKT Ruvu na Ruvu Shooting kucheza saa 10.30 jioni siku hiyo hiyo.
Novemba 17, Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City saa 8.00 mchana wakati Majimaji itacheza na Mtibwa saa 10.30 jioni.
Ligi hiyo ya mkondo mmoja, hatua ya makundi inatarajiwa kufikia ukomo Desemba 12, 2016 ambako timu nne vinara kutoka katika kila kundi zitapangiwa ratiba mpya na kituo ili kutafuta bingwa wa msimu kwa timu za vijana.
Kituo hicho kitatangazwa baada ya kumalizika hatua ya makundi hapo Desemba 12, mwaka huu.
Ujio wa ligi hiyo ni utekelezaji au kukidhi matakwa ya maelekeo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika kategori ya uwepo wa timu za vijana zinazoshindana mbali ya kupata huduma za shule na matibabu kwa timu zote za Ligi Kuu na Ligi daraja la Kwanza.