Mzunguko wa tano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
(VPL) unaendelea leo kwa mchezo kati ya
African Lyon ya Dar es Salaam na Toto African ya Mwanza kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam. African Lyon inaingia uwanjani ikiwa na
kumbukumbu nzuri ya kuilaza Mbao FC mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Uhuru,
Dar es Salaam wakati Toto African ilitoka kufungwa 1-0 na Tanzania
Prisons ya Mbeya.
Raundi ya sita utapigwa Septemba 24, 2016 na Septemba 25, 2016 kwa
michezo mitano siku ya Jumamosi na mitatu siku ya Jumapili. Siku ya
Jumamosi JKT Ruvu itaikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Mabatini
ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Simba itakuwa mwenyeji wa Majimaji
ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Azam FC itasafiri hadi Mtwara kwenda kucheza na Ndanda kwenye Uwanja
wa Nangwanda Sijaona wakati Mwadui ya Shinyanga itakuwa mgeni wa
Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Mtibwa Sugar
itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Manungu ulioko
Turiani mkoani Morogoro.
Siku ya Jumapili, Septemba 25,
mwaka huu Ruvu Shooting inatarajiwa kuikaribisha Toto African kwenye
Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikiwa
mwenyeji wa Young Africans katika dimba la CCM Kambarage wakati Kagera
Sugar itakuwa jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru ikicheza na
African Lyon.
No comments:
Post a Comment