Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 22, 2016

SHIME ATOA LA MOYONI KUHUSU SERENGETI BOYS


img_3864
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Bakari Shime amewatoa shaka baadhi ya mashabiki wa wasoka walioonesha kukata tamaa na matarajio ya kikosi chake ambacho mwishoni mwa mwezi huu kitakabiliwana mchezo muhimu wa kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana dhidi ya Congo Brazzaville.
Shime amesema watanzania wote kwa pamoja bado wanatakiwa kuiamini timu yao kutokana na kuwa na mikakati mziuri ya kwenda ugenini na kupata ushindi kama ilivyokua kwenye michezo iliyotangulia.
Amesema yeye kama kocha hana shaka kutokana na kuamini hakuna litakaloshindikana katika mchezo wa mkondo wa pili, hasa ikizingatiwa tayari kuna baadhi ya madhaifu ya timu pinzani ameshayasoma na kuyatafutia mbinu.
“Niwatoe wasiwasi watanzania, sisi tumekuwa tukijiandaa kushinda kila wakati. Tumecheza mechi yetu tumeshinda, tunakwenda kucheza ugenini inabidi tushinde na tuvuke.”
“Tunafuraha wa safu ya ulinzi watakuwepo mchezo baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kadi. Hali ya golikipa wetu inaendelea vizuri sana na naamini ataanza mazoezi.”
“Tunakwenda kupambana kwenye mchezo ule, itakuwa ni vita naamini serikali inamkono mrefu inaweza kufanya kila kitu.”