Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba (kulia) akikimbizwa na kiungo wa Leicester City, Danny Drinkwater wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika leo mchana kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester, kaskazini magharibi ya London. Man United ilishinda mabao 4-1. |
TIMU
ya Manchester United leo imeutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Old
Trafford baada ya kuwafunga mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England Leicester
City kwa mabao 4-1.
Wakati
timu hiyo ikiibuka na ushindi mnono, kocha Jose Mourinho amemuacha kando ya
kikosi cha kwanza nahodha wake Wayne Rooney.
Chris
Smalling ndiye alikuwa wa kwanza kuipatia bao Man United kabla Juan Mata
hajafunga la pili na kuifanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 2-0.
Marcus
Rashford na Paul Pogba wamefunga mabao yao ya kwanza katika timu hiyo,
ambapo yote yalifungwa kwa njia ya kona.
Mabingwa
watetezi Leicester City wenyewe walipata bao lao la kufutia machozi
lililofungwa na Demarai Gray kwa shuti la mbali.
Rooney
aliingia uwanjani katika dakika ya 83.
No comments:
Post a Comment