Mshambuliaji mwenye mafanikio na soka la Tanzania na pia mwenye rekodi pekee ya kucheza timu kubwa tatu nchini ambazo ni Yanga,Azam na Simba,Mrisho Khalifani Ngassa hata hivyo ameweza kuvitumikia vilabu vya kanda ya Ziwa,Scad Magu ya Magu,Toto African ya Mwanza na Kagera Sugar ya Kagera kwa nyakati tofauti ameamua kuvunja mkataba wake na klabu ya Free State.
Ngassa alikutana uongonzi wa timu hiyo na kukaa kikao kizito chini ya Meneja,Rantsi Mokoena hivyo pande zote mbili zilikubaliana kuwa mchezaji huyu avunje mkataba na wao kama timu wanaheshimu maamuzi ya mchezaji huyu mwenye rekodi ya kuwa mfungaji bora wa michuano ya klabu bingwa Afrika akiwa na timu ya Yanga.
“Ni kweli Ngassa tumekubaliana naye kuvunja mkataba kwani alikuwa na mashiko yake na yalikuwa na msingi hivyo tunamshukuru kwa muda ambao tumekaa naye alikuwa mchezaji mzuri kwetu ameweza kutusaidia hivyo tunamtakia maisha mema na mafanikio”alisema Mokoena.
Hoja kubwa ambayo inasemekana Ngassa kuamua kuvunja mkataba na timu hiyo ni kwamba Free State hawana malengo na kushinda taji na yeye malengo yake ni kutwaa makombe mbalimbali wao wapo kwa ajili ya kushiriki Ligi tu bila kuwa na malengo na mafanikio hii ndio hoja kubwa.
Free State tayari wameshaingia na Mkataba na mshambuliaji hatari wa zamani wa Yanga na Simba,Hamis Kiiza,walioingia naye kwa mkataba wa miaka minne pengine Ngassa ameamua kumkimbia Kiiza kutokana na uimara wa kufumania nyavu,Kiiza alikuwa mchezaji wa Simba msimu uliopita na aliweza kufunga magoli 19 nyuma ya mfungaji bora wa ligi Amis Tambwe ambaye alifunga magoli 21 akiwa na Yanga na mwaka huu wekundu wa msimbazi wameweza kuachana naye kutokana kuwa na nidhamu mbovu.
Add caption |
No comments:
Post a Comment