Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, August 18, 2016

SADIO MANE AUMIAMAZOEZINI, AKIMBIZWA HOSPITALI KUCHUNGUZWA BEGA LAKE


LEO mchezaji mpya wa Liverpool Sadio Mane alikimbizwa Hospitalini kutibiwa na kuchunguzwa Bega lake baada ya kuumia Mazoezini.
Mane, aliesainiwa kwa Pauni milioni 30, ilibidi aharakishwe Hospitalini baada ya kuumia alipogongona na Mchezaji mwenzake wakati wa Mazoezi kwenye Kituo chao cha Mazoezi cha Melwood huko Jijini Liverpool.

Mane, Raia wa Senegal, aling’ara mno Jumapili iliyopita akicheza Mechi yake ya kwanza kwa Klabu yake mpya Liverpool walipoichapa Arsenal 4-3 huko Emirates kwenye Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England Msimu huu mpya wa 2016/17 huku yeye akifunga Bao tamu.

Baada ya kufunga Bao hilo, Mane alimrukia Mgongo Meneja wao Jurgen Klopp wakisherehekea.

Mechi inayofuata kwa Liverpool ni hapo Jumamosi ikiwa ni Ugenini tena na Burnley na hii ni Mechi yao ya pili mfululizo kucheza Ugenini kwenye Ligi Kuu England na hilo ni kwa makusudi tu kutokana na maombi yao wenyewe ili kupisha ujenzi wa upanuzi wa Jukwaa Kuu la Uwanja wao wa Anfield.