Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, August 18, 2016

OLIMPIKI RIO 2016: NEYMAR APIGA BAO, BRAZIL IKIWANYUKA WENZAO 6-0, SASA FAINALI

WAKIWA kwao Maracanã - Estádio Jornalista Mário Filho Jijini Rio De Janeiro, Brazil wametinga Fainali wakiwania Medali yao ya Kwanza kabisa ya Michezo ya Olimpiki baada ya kuwatwanga Honduras Bao 6-0.
Brazil walianza Mechi hii kwa kishindo kikubwa pale Kepteni wao Neymar alipofunga Bao lao la kwanza baada ya Sekunde 14 tu tangu Mechi ianze ikiwa ni Historia kwa Olimpiki kwa Bao la haraka kiasi hicho.
Hata hivyo Neymar alileta kutaharuki Uwanjani baada ya kuumia akifunga Bao hilo alipogongana na Kipa Luis Lopez na kutolewa nje kwa Machela.
Neymar aliweza kurudi tena Uwanjani lakini muda mfupi baadae akakaa chini kwa maumivu na kutolewa tena nje lakini akaweza kurudi tena na kuendelea tena na Mechi.
Brazil waliongeza Bao 2 katika Dakika za 26 na 35 kupitia Gabriel Jesus.
Hadi Mapumziko Brazil 3 Honduras 0.
Kipindi cha Pili Brazil walipiga Bao 3 nyingine za Dakika za 51, 79 na 90 ambalo lilikuwa la Penati.
Bao hizo zilifungwa na Marquinhos, Luan na Neymar kwa Prnati.
Brazil sasa watacheza Fainali na Mshindi kati ya Nigeria na Germany ambao wanacheza baadae Leo.