Kampuni
ya MultiChoice Tanzania imesaini mkataba wa mwaka mmoja na mwanariadha
Alphonce Felix Simbu aliyeshiriki mashindano ya Olympic ya Rio 2016
yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini Brazil na kushika nafasi ya 5
kati ya wanariadha 157 kwenye mbio za Marathon za wanaume.
Katika
Mkataba huu, Kampuni ya Multichoice Tanzania imemzawadia Alphonce Simbu
shillingi za Kitanzania 1,000,0000 ambazo atalipwa kila mwezi kwa
kipindi cha mwaka mmoja lengo likiwa ni kumsadia katika maandalizi yake
ya mashindano yajayo ya IAAF WORLD CHAMPIONSHIP yanayotarajiwa kufanyika
mjini London Uingereza August 2017.
Vile
vile bwana Alphonce Simbu atapatiwa vifaa maalumu vya kuumuwezesha
kufanya mazoezi yake vyema. Vifaa hivi ni kama vile, viatu na nguo za
mchezo wa Riadha.
Mwanariadha
aliyeshiriki mashindano ya Olympic ya Rio 2016, Alphonce Felix Simbu
akisaini mkataba na Kampuni ya Multichoice Tanzania. Kulia anayeshuhudia
tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande.
Si
hivyo tu bali Kampuni ya MultiChoice itamtengenezea makala yenye
kuonyesha matukio mbalimbali aliyopitia ya Kimichezo na Familia siku za
nyuma. Vile vile watarekodi mazoezi atakayofanya akiwa katika kambi ya
riadha Chuo cha Wakala wa Mistu Fiti kilichopo West Kilimanjaro eneo la
Ngarenairobi Wilaya ya Sia Mkoa Kilimanjaro. Makala hii itarushwa kwenye
DStv hapo baadae.
Katika
Kipindi hicho cha mkataba huu Alphonce Felix Simbu atakuwa Balozi wa
Kampuni ya MultiChoice Tanzania ambapo atashiriki katika promosheni
mbalimbali kutangaza huduma zake.
Alipokuwa
akisaini mkataba huo Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania, Maharage
Chande mbele ya Rais wa Riadha Tanzania na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mh.
Anthony Mtaka, mwalimu wake Alphonce Nd. Francis John Marcially pamoja
na Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, alisisitiza
kuwa “huu ni mwanzo na kadri mafanikio yanavyoongezeka Multichoice
itakuwa tayari kuwa mstari wa mbele kushirikiana na chama cha riadha
Tanzania katika kunyanyua riadha Tanzania na kurudisha heshima ya taifa
kwenye mchezo huo”.
Mkurugenzi
Mkuu wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (wa pili kulia aliyeketi)
akimkabidhi nakala ya mkataba Mwanariadha aliyeshiriki mashindano ya
Olympic ya Rio 2016, Alphonce Felix Simbu. Wengine katika picha ni Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mh. Anthony Mtaka (kushoto) na Meneja Masoko wa
MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu.
No comments:
Post a Comment