Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 31, 2016

ARSENAL YAMRUHUSU WILSHERE KUONDOKA KWA MKOPO

Arsenal wako tayari kumruhusu Kiungo wao wa England Jack Wilshere kuondoka kwenda kuchezea Klabu nyingine kwa Mkopo.
Wilshere, mwenye Miaka 24, amekuwa akikumbwa na majeruhi ya mara kwa mara kiasi cha Msimu uliopita kuichezea Arsenal Mechi 3 tu baada ya kuvunjika Mguu wa Kushoto.
Baada ya Msimu huo kwisha, Wilshere aliichezea England Mechi 6 zikiwemo Mechi 3 za kwenye Fainali za EURO 2016 huko France Mwezi Juni na Julai.
Lakini Jana hakuwemo kwenye Kikosi cha England cha Wachezaji 23 kilichotangazwa na Meneja mpya Sam Allardyce kwa ajili ya Mechi zao za Kundi F la kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Kwa ajili ya Msimu huu mpya, Arsenal ililipa Pauni Milioni 35 kumnunua Kiungo wa Switzerland Granit Xhaka.
Wilshere, ambae ameichezea England mara 34 na Gemu 80 za Ligi Kuu England akiwa na Arsenal, ameingizwa Gemu 2 tu za Ligi Msimu huu akitokea Benchi kuichezea Arsenal.
Mwaka 2010, Wilshere aliwahi kwenda Bolton Wanderers kucheza kwa Mkopo.
Wilshere ana muda hadi kesho Usiku kuamua wapi aende kwa Mkopo kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa rasmi.
You might also like:
FULL TIME: MANCHESTER CITY 2 v 3 ARSENAL
FULL TIME: FULHAM 1 v EVERTON 3