Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, July 28, 2016

CHELSEA KUMWAGA £38M KWA BEKI WA NAPOLI KALIDOU KOULIBALY

SASA Minoti tu inatembezwa na Vigogo wa England katika harakati zao za kujiimarisha baada kuibuka ripoti kuwa Chelsea imetayarisha Daul la Pauni Milioni 38 kumnasa Beki wa Napoli ya Italy Kalidou Koulibaly wakati Manchester City ikiwa mazungumzoni kuilipa Everton Pauni Milioni 50 kumchukua Beki John Stones.

KALIDOU KOULIBALY
Kwa mujibu wa Sky Italy Chelsea imetoa Ofa ya Pauni Milioni 38 kumnunua Beki wa Napoli, Kalidou Koulibaly, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa Senegal mwenye Miaka 25.

Wakala wa Koulibaly, Bruno Satin, amethibitisha nia ya Chelsea huku Mchezaji mwenyewe akitoa shinikizo kwa kukataa kusaini Mkataba mpya na Napoli.

Satin ameeleza kuwa wanapaswa kuondoka Napoli kwa sababu za kiuchumi tu na kile kilichotokea kwa Gonzalo Higuain, ambae aliihama Napoli kwenda Juventus, ambao ni Wapinzani wengine humo humo Italy, hakitatokea.

Koulibaly alijiunga na Napoli kutoka Genk ya Ubelgiji Mwaka 2014 na kwa sasa ana Mkataba na Napoli hadi 2019.

Akiwa na Napoli aliichezea Mechi 60 kwenye Serie A na kufunga Bao 1 huku pia akiwahi kuichezea U-20 ya France kabla kuamua kuwakilisha Nchi yake Senegal katika ngazi za juu.

Ikiwa atatua Chelsea, atakuwa Mchezaji wa 3 kusainiwa na Meneja Mpya Antonio Conte ambae pia amewanunua Straika Michy Batshuayi na Kiungo N'Golo Kante.