Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, June 25, 2016

SHELISHELI YAIHOFIA SERENGETI BOYS


     Kocha wa timu ya Taifa ya soka ya Vijana (U-17) Bakari Shime  (kulia) akiongea na wandishi wa habari kuhusu mchezo wa kuwania kufuzu fainali za vijana Afrika utakaochezwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katikati ni kocha wa timu ya Shelisheli, Gavin Jeanne na Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas. (Picha na Rahel Pallangyo)


KOCHA wa timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti boys’ Bakari Shime,  amejigamba kuifunga Shelisheli katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika utakaochezwa leo kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku wapinzani wakionekana kuihofia Serengeti.
Akizungumza leo wakati wa mkutano na wandishi wa habari, Shime alisema wamefanya maandalizi ya kutosha na kikosi chake hakina majeruhi hivyo anawaahidi watanzania kupata burudani ya uhakika.
“Tunashukuru shirikisho limetupatia maandalizi mazuri na kikosi hakina majeruhi hivyo naamini ushindi ni muhimu ili tuweze kujiweka pazuri kufuzu fainali hizi”, alisema Shime.
Naye Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Shelisheli, Gavan Jeanne ameonesha kuihofia Serengeti Boys kutokana na maandalizi ambayo wameyapata huku akiutaja mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri ambao Serengeti ilicheza na kushinda na safari ya India.
“Hatujawahi kushiriki michuano ya vijana, hivyo hii ni mara yetu ya kwanza na tunajua Serengeti boys wameandaliwa vizuri kwani wamecheza na Misri na wamefanya ziara ya kimichezo India lakini mchezo hatutakubali kufungwa kirahisi”, alisema Jeanne.
Mchezo huu utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia, ambao ni Belay Tadesse Asserese akisaidiwa na  Tigle Gizaw Belachew na Kinfe Yilma Kinfe na mezani atakuwepo Lemma Nigussie huku Kamishna wa akiwa Bester Kalombo.
Serengeti Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo wa leo na marudiano  ni Julai 2, 2016 huko Shelisheli endapo Serengeti boys itafanikiwa kuiondoa Shelisheli itakutana na Afrika Kusini kwenye hatua ya pili
Katika kuhakikisha hamasa inakuwepo kwa Serengeti boys, Shirikisho la Soka nchini, jana limeiondoa kwenye hostel za Karume na kuwapeleka kwenye hotel ya Urban Rose iliyopo katikati ya jiji.