Siku kadhaa baada ya Manchester United kumfukuza aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Louis Van Gaal na kumchukua kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho, nahodha wa Man United, Wayne ametoa maoni yake kumhusu kocha huyo
Rooney alimtaja Mourinho kama moja ya makocha bora na anaamini katika uwezo wake hivyo anaamini ataweza kuisaidia klabu hiyo kurudi katika ubora ambao ilikuwa nao awali.
“Ni moja kati ya makocha bora duniani na anaijua vizuri Ligi Kuu ya Uingereza. Kwangu na hata wachezaji wengine wa Manchester United huu ni muda mwafaka. Nalisubiri kwa hamu,” alisema Rooney.