Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 23, 2016

VPL MSIMU 2015/2016 WAMALIZIKA TANZANIA, TIMU ZA TANGA TATU ZASHUKA DARAJA, KUCHEZA DARAJA LA 1

Picha chini ni Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga wakifurahia Kagera Sugar kuwanyuka Mwadui FC bao 2-0.VPL, Ligi Kuu Vodacom, Leo imefikia tamati kwa Msimu wa 2015/16 kwa Mechi zake za mwisho huku Bingwa akiwa amepatikana mapema baada ya Yanga kutetea vyema Taji lao na kuacha kimbembe kwa hasa nani atashuka Daraja kuungana na Coastal Union.

Matokeo ya hii Leo yamezishusha Timu zote za Tanga, African Sports na Mgambo JKT, ambao sasa wataungana na mwenzao wa Tanga Coastal Union kucheza Daraja la Kwanza Msimu ujao.
Timu 3 zilizopanda Daraja na kuchukua nafasi ya hizo 3 ni Ruvu Shooting, Mbao FC na African Lyon.

LIGI KUU VODACOM
MATOKEO:
Jumapili Mei 22

Mbeya City 0 vs Ndanda FC 0
Coastal Union 0 vs Tanzania Prisons 2
Simba 1 vs JKT Ruvu 2
Toto Africans 0 vs Stand United 1
Azam FC 1 vs Mgambo JKT 1
Kagera Sugar 2 vs Mwadui FC 0
Mtibwa Sugar 2 vs African Sports 0
Majimaji 2 vs Yanga 2

No comments:

Post a Comment