Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 11, 2016

RENATO SANCHES NA MATS HUMMELS WASAINI BAYERN MUNICH


MABINGWA wa Germany Bayern Munich wamemsaini Mchezaji wa Borussia Dortmund Mats Hummels na wa Benfica Renato Sanches kwa ajili ya Msimu mpya ujao.
Hummels, mwenye Miaka 27, atajiunga na Bayern kwa dili ya Miaka Mitano endapo atafuzu upimwaji afya yake huku Dau likifichwa na Klabu zote mbili.

Bayern vile vile wamenunua Kiungo wa Benfica ya Portugal, Renato Sanches mwenye Miaka 18 kwa Dau la Euro Milioni 35 ambalo huenda likapanda hadi kufikia Euro Milioni 45 ikiwa vigezo kadhaa vitafikiwa.
Renato alipimwa afya yake Jana na kusaini Dili ya Miaka Mitano.
Wachezaji hao Wawili watakuwa chini ya Meneja mpya Carlo Ancelotti anaechekua wadhifa kutoka kwa Pep Guardiola ambae amejiunga na Manchester City kwa ajili ya Msimu unaokuja.

Hummels atakuwa akirejea tena Klabu yake ya zamani Bayern ambayo aliichezea Mechi moja tu ya Bundesliga Mwaka 2007 kabla ya kuhamia Dortmund Timu ataichezea kwa mara ya mwisho hapo Mei 21 kwenye Fainali ya Kombe la Germany, DFB Pokal, dhidi ya Timu yake mpya Bayern Munich.