Tamasha la Filamu la Zanzibar (ZIFF) linataraji kuanza mwezi Julai, 9 hadi Jula, 17 huku filamu 80 zikitarajiwa kushiriki katika tamasha hilo kubwa la filamu visiwani Zanzibar.
Akizungumzia tamasha hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF, Martin Muhando amesema kuwa kwa mwaka 2016 walipokea maombi ya filamu 490 ambazo ziliomba kushiriki tamasha hilo lakini wamepitisha filamu 80 ambazo zitakuwa katika vipengele vitano.
“Wachambuzi wamechagua makundi matano, kutakuwa na kundi la filamu za kawaida litakuwa na filamu 59, Sembene Ousmmane 15, Filamu za Tanzania 12 na filamu tano zitakuwa zinahusu Zanzibar na mshindi atapata tuzo ya Emerson,” amesema Muhando.
DSC_1077
Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF, Martin Muhando akizungumzia tamasha la mwaka huu. Kulia ni Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi na Lilian Lundo kutoka Habari Maelezo.
Amesema kwa mwaka huu maombi yaliongezeka ambapo filamu za Tanzania walipokea 40 na kati ya hizo tano zitashindana katika kipengele cha Ousmmane na kiujumla Tanzania imeingiza filamu 8, Kenya 5, Uganda  3 na Kenya.
Aidha aliongeza kuwa katika tamasha la mwaka huu kutakuwa mashindano ya video za muziki na kutakuwa na filamu mpya tatu ambazo hazijaambulishwa sehemu yoyote na katika ZIFF ndiyo itakuwa sehemu ya kwanza.
DSC_1074
Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi akizunguzia mabadiliko ya tamasha kwa mwaka 2016. Kulia ni Meneja Mtendaji wa ZIFF, Martin Muhando na Zuhirah Khaldun kutoka Diarra.