Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 5, 2016

AZAM MAJANGA, SIMBA SASA NAFASI YA PILI

 Azam-JKT Ruvu
Azam FC imepokwa pointi tatu na mabao matatu kutokana na kumtumia beki wao, Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema katika mechi namba 156 iliyozikutanisha Mbeya City dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Azam ilimchezesha Nyoni kinyume na sheria huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
“Azam wamepoteza mchezo huo na sasa Mbeya City imepewa pointi tatu na mabao matatu, pia tumewapa onyo benchi la ufundi la Azam kuwa makini ili jambo hili lisitokee tena,” amesema afisa habari wa TFF Alfred Lucas.
Kwa matokeo hayo sasa Simbsa inashika nafasi ya pili huku Yanga wakiendelea kuongoza ligi.

No comments:

Post a Comment