Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, March 7, 2016

WAZIRI NAPE AIAGA TIMU YA MAGONGO INAYOKWENDA NAMIBIA KWENYE MASHINDANO YA AFRIKA
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameiaga timu ya Taifa ya vijana U-21 ya mchezo wa Magongo inayokwenda kushiriki mashindano ya Ubingwa wa Afrika yatakayofanyika Windhoek, Namibia kuanzia Machi 18-28.
Akizungumza kabla ya kukabidhi bendera pamoja na vifaa vya michezo vilivyotolewa na benki ya NMB, Nape aliwataka wachezaji hao kwenda kutetea bendera ya Tanzania kwani wanamichezo waliopita wizarani hapo wamekuwa wakifanya vizuri.
“Naamini mtakwenda kushindana ili kutetea heshima ya nchi yetu na naamini mtafuata nyayo za wanamichezo wengine waliopita hapa wizarani,” alisema Nape.
Pia Nape alisema wizara yake imeajiandaa kuhakikisha michezo yote inapewa kipaumbele na kuwaomba NMB kuogeza udhamini kutoka mwaka mmoja hadi miaka mitatu au mitato ili kuweo na uhakika wa kujiandaa mapema.
Mashindano hayo ya Magongo ya timu za vijana yatashirikisha timu za mataifa saba ambazo ni Namibia, Afrika Kusini, Kenya, Botswana, Nigeria, Zimbabwe na Tanzania ambapo ni mara ya kwanza ikishiriki.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Magongo, Abraham Sykes alisema timu hiyo inatarajiwa kuondoka Machi 13 kwa basi kutokana na ukata unaoikabili chama chao.