Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, March 2, 2016

ARSENAL WAPATA PIGO , ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN NJE

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema Kiungo wao Alex Oxlade-Chamberlain atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 6 hadi 8 lakini hahitaji upasuaji baada ya kuumia Goti walipofungwa 2-0 na Barcelona Februari 23 kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Oxlade-Chamberlain, mwenye Miaka 22, alilazimika kuondoka Uwanjani Emirates mara baada ya kufungwa na Barca huku akitumia msaada wa Magongo kutembelea.
Arsenal, ambao walichapwa 3-2 na Man United Jumapili iliyopita huko Old Trafford kwenye Ligi Kuu England, Jumatano Usiku wako kwao Emirates kucheza na Swansea City Mechi ya Ligi.Arsenal wapo Nafasi ya 3 kwenye Ligi wakiwa Pointi 3 nyuma ya Tottenham na Pointi 5 nyuma ya Vinara Leicester City.
Wakitoka kwa Swansea City, Arsenal wana kibarua kigumu huko White Hart Lane kwenye Dabi ya London ya Kaskazini dhidi ya Mahasimu wao wa Jadi, Tottenham hapo Jumamosi Machi 5.