VITA ya kuwania kupanda Ligi Kuu kwa
timu za Kundi C inaendelea leo, ambapo Geita Gold FC itakuwa mwenyeji wa JKT
Oljoro, mchezo ambao unatabiriwa kuwa
mgumu.
Mchezo huo utachezwa Shinyanga utavuta hisia za mashabiki wengi kwani timu
ambayo itapoteza mchezo huo itajiweka kwenye wakati mgumu wa kupanda ligi Kuu.
Geita ina pointi 24 sawa na Polisi
Tabora wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufunga inacheza na JKT
Oljoro yenye pointi 22.
Endapo JKT Oljoro itashinda mchezo
huo itaipita Geita kwa pointi moja kitendo ambacho kitasababisha michezo ya
mwisho kuwa migumu.
Vita ya kupanda kwenye kundi C
inajumuisha Polisi Tabora ambao wana pointi 24 ambao leo watakuwa wageni wa JKT
Kanembwa yenye pointi tatu mchezo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Lake
Tanganyika.
Pia Polisi Mara itaikarisha Panone
FC kwenye Uwanja wa Karume, Mara, mchezo ambao hauna msisimko kwani timu Panone
wana pointi 15 na Polisi pointi 12 jambo linalowatoa kwenye mbio za kuwania kupanda
daraja.
Kwenye kundi A, Ashanti United
ambayo ina pointi 22 itacheza na KMC FC
yenye pointi 2, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na African
Lyon yenye pointi 23 wanaikarisha Polisi Dar yenye pointi 14 mchezo unaochezwa
Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Timu yoyote kati ya Ashanti United,
KMC FC, African Lyon endapo itapoteza mchezo leo itajiweka pabaya kwenye mbio
za kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Michezo mingine kundi A itachezwa
kesho ambapo Friends Rangers itaialika Mji Mkuu, kwenye Uwanja wa Karume, Dar
es Salaam na Kiluvya United dhidi ya Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Mabatini
Pwani
Michezo mingine ambayo ni ya
kukamilisha ratiba itakayochezwa leo ni ya kundi B, kwani Ruvu Shooting
walishapanda ni kati ya Polisi Morogoro itakayoikaribisha Njombe Mji kwenye
Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Kurugenzi FC wataikarisha JKT Mlale,
Burkinafaso FC wataialika Lipuli FC na Kimondo FC wataikaribisa Ruvu Shooting,
huko Vwawa Mbozi.
No comments:
Post a Comment