Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 1, 2016

DJIKOVIC AIBUKA KIDEDEA KWA KUMLAZA MURRAY

Mchezaji tenis anayeorodheshwa nambari moja duniani kwa upande wa wanaume Novak Djokovic amemlaza Andy Murray na kuibuka mshindi wa taji la Australia la mchezo huo.
Mserbia mwenye umri wa miaka 28 alithibitisha udedea wake alipomlamza Murray seti tatu kwa nunge za alama 6-1 7-5 7-6 (7-3).

Kichapo hicho ni cha 5 kwa muingereza Murray ambaye sasa ameshindwa katika fainali zote 5 alizowahi kushiriki za mchuano wa wazi wa Australia.
4 kati ya hizo mikononi mwa mtani wake wa jadi Djokovic .
Kwa upande wake Djokovic alisajili ushindi wake wa 6 mjini Melbourne na sasa anatoshana nguvu na bingwa wa zamani Roy Emerson kutoka Australia.

Djokovic vilvile ametoshana makali na vigogo wa mchezo huo Bjorn Borg na Rod Laver waliowahi kushinda mataji 11 ya Grand Slam.
Murray, 28, sasa ameingia katika kumbukumbu kwa kushindwa katika fainali 5 za Grand Slam za tenis tangu kuasisiwa kwa mashindano hayo ya wazi mwaka wa 1968.
Murray alifululiza moja kwa moja hadi kwenye uwanja wa ndege ambapo anatarajiwa kujiunga na mkewe anapojifungua wakati wowote kutokea sasa.

 Djokovic ameshinda mataji 4 kati ya tano makuu ya tenis ikiwemo 3 mfululizo.
Endapo Mserbia huyo atashinda mashindano ya wazi ya Ufaransa mnamo mwezi juni basi ataweka rekodi ya kushinda mataji yote makuu msimu huu.

No comments:

Post a Comment