Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 2, 2016

UHAMISHO JANUARI WAANZA KWA KASI, BOUREMOUTH YAMSAJILI ITURBE, VAN GAAL KUNUNUA STRAIKA, CHELSEA, ARSENAL KUINGIA USWISI, ITALIA KUNASA MASTAA

WAKATI Klabu ya Bournemouth ikiingia Sokoni kumchukua Kiungo wa AS Roma Juan Manuel Iturbe kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu, Meneja wa Man United Louis van Gaal anatafakari kununua Straika ili kunoa Fowadi yake butu huku ripoti zikidai Chelsea na Arsenal zina nia ya kuchukua Mastaa kutoka Uswisi na Italy. Juan Manuel Iturbe
Iturbe, mwenye Miaka 24 na ni Mchezaji kutoka Argentina, ilikuwa nusura aende Watford lakini Bournemouth wakatia mkono haraka na kumchota.
Stamford Bridge
Kutoka Stamford Bridge, zipo ripoti kuwa Chelsea inataka kumnunua Straika wa FC Basel Breel Embolo mwenye Miaka 18 ili kuziba pengo la Loic Remy na Radamel Falcao ambao wanatarajiwa kuondoka Mwezi huu Januari.
Inasemekana FC Basel wako tayari kumuuza Embolo ikiwa Chelsea watatoa Pauni Milioni 20.
Embolo huichezea Timu ya Taifa ya Switzerland na ameifungia FC Basel Bao 16 katika Mechi 47 za Ligi.
Emirates
Nao Arsenal wanadaiwa kuwa na nia ya kumsaini Straika wa Napoli Lorenzo Insigne mwenye Miaka 24.
Wakala wa Insigne, Antonio Ottaiano, ameiambia Radio Kiss Kiss Napoli kuwa Paris Saint-Germain na Arsenal zimeonyesha nia ya kumsaini Straika huyo.
Old Trafford
Huku wakitoka kwenye Mwezi mbovu kabisa katika Historia yao ya Miaka 138, Meneja wa Manchester United Louis van Gaal sasa anataka kununua Straika katika Dirisha la Uhamisho la Mwezi huu Januari.
Wakiwa wamefunga Bao 25 tu katika Mechi zao 25 zilizopita na pia kuambua Sare 7 za bila Magoli Msimu huu, 6 zikiwa Uwanjani Old Trafford, na pia kufungwa katika Mechi zao 4 zilizopita, 3 zikiwa za Ligi, Van Gaal ameona Straika mpya ndio Mwarobaini wa tatizo lao.
Hivi sasa tegemezi kubwa kwa ufungaji kwa Man United ni Kepteni wao Wayne Rooney na Anthony Martial ambao Msimu huu kila mmoja amefunga Bao 7.
Ijumaa, Van Gaal alifupisha Mkopo wa Chipukizi Will Keane, mwenye Miaka 22, kwa Preston na kumrudisha Old Trafford ili kuimarisha mashambulizi.
Van Gaal ametamka: “Kufunga Mabao ni kipaji. Tunacho hicho kipaji lakini Wachezaji hawajiamini hivi sasa na pengine itabidi tununue Straika mwingine!”
Akielezea matatizo yao, Van Gaal alisema: “Tatizo letu ni ufungaji. Ukitathmini Mechi zetu zote utaona tumeweza kucheza Staili yetu. Ukiondoa Mechi na Arsenal, na Kipindi cha Kwanza dhidi ya Stoke na Palace, hizo hatukucheza Mpira wetu.”
Man United walifungwa na Arsenal na Stoke na kutoka Sare na Palace.
Aliongeza: “Mechi zote zilizobaki tulicheza Mpira wetu na kutengeneza nafasi, kutawala lakini hatukufunga. Tunahitaji pia Straika awe na bahati. Wachezaji wengi hucheza nafasi hiyo na wanapata nafasi ya kufunga na hawafungi, huweza kueleza hilo.”
Mwanzoni mwa Msimu huu, Van Gaal aliruhusu Mastraika Wawili kuuzwa, Javier Hernández kwenda Bayer Leverkusen na Robin van Persie kwa Fenerbahce na kuruhusu Radamel Falcao kuondoka baada ya Mkopo wake kwisha na pia kumtoa Chipukizi James Wilson kwenda Mkopo huko Brighton & Hove Albion

Van Gaal amesema: “Tungeweza kuwabakisha Mastraika wote lakini tungekuwa na Mastraika wengi kwenye Benchi. Watakosa furaha na kutaka kuondoka. Hiyo ndio hadithi ya Chicharito. Anataka kucheza”

No comments:

Post a Comment