Nahodha wa timu ya taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ na klabu ya soka ya Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ameamua
kustaafu kuichezea timu hiyo ili kuweka nguvu kwenye klabu yake Yanga.
Jambo jingine Cannavaro amesema ni lawama anazopata kutoka kwa mashabiki ambao wanadai yeye ndiye anayeifungisha timu hiyo pale inapopata matokeo mabovu.
Cannavaro anasema maneno yamekuwa mengi na yalianza mara baada ya mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Algeria kule kwao.
“Katika mechi hiyo tulifungwa mabao 7-0, mechi hiyo muda mwingi tulijitahidi kupambana kuhakikisha tunawatoa Algeria lakini ikashindikana, cha ajabu mara baada ya mechi hiyo nilionekana mimi pekee ndiye niliyefungisha”, alisema Cannavaro.
Cannavaro kwa sasa ameamua kujiweka pembeni baada ya kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa kumtangaza Samatta kama nahodha mpya.
Cannavaro amesema amepeleka barua rasmi kwa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF ya kuwapa taarifa ya kustaafu kwake kuichezea timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment