RAIS wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za
pongezi mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kufuatia kuteuliwa kuwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika serikali ya awamu ya tano.
Akizungumza na gazeti hili, Malinzi alisema
kuwa amempongeza Nape kwani TFF ina imani nae katika nafasi hiyo, na kuahidi
kushirikiana katika michezo na haswa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya
mpira wa miguu nchini.“Sisi tuna imani nae hivyo nawaomba wanamichezo wampe sapoti ili aweze kutimiza majukumu yake kisawasawa. Pia nawapongeza wanamichezo wengine ambao wamechaguliwa katika nyadhifa mbalimbali katika chaguzi zilizofanyika na zinazoendelea”, alisema Malinzi
Malinzi amewapongeza Paschal Kihanga, Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa hiyo, na James Bwire mmiliki wa shule ya Alliance kwa kuchaguliwa meya wa manispaa ya Nyamgana.
Amewatakia kila la kheri katika nafasi hizo walizozipata za kuwatumikia watanzania, na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini anawaahidi kushirikiana nao.
No comments:
Post a Comment