Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 21, 2015

LIONEL MESSI NA SUAREZ WAIPATIA BARCELONA KOMBE LA FIFA KWA KLABU BAADA YA KUIFUNGA RIVER PLATE 3-0

Ndani ya Uwanja wa Yokohama International

Barca waliofunga bao ni
 Lionel Messi 36' 

 Luis Suárez 49'
Luis Suárez 68.

MABINGWA wa Ulaya, FC Barcelona, Leo wamebeba Kombe la Dunia kwa Klabu huko International Stadium Yokohama, Jijini Yokohama, Japan baada ya kuifunga River Plate ya Argentina Bao 3-0.
Hili ni Kombe la 5 kwa Barca kutwaa kwa 2015 baada ya kuyazoa La Liga, UEFA CHAMPIONS LIGI, Copa del Rey na lile la Ulaya la Super Cup na hili ni Kombe lao 3 la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.
Bao za Barca zilifungwa na Lionel Messi, na kudumu hadi Haftaimu, na nyingine za Kipindi cha Pili za Luis Suarez.
Katika Mechi ya awali ya kusaka Mshindi wa 3, Wenyeji Sanfrecce Hiroshima walitoka nyuma na kuipiga Guangzhou Evergrande Bao 2-1.
Magoli ya Sanfrecce Hiroshima yalifungwa na Douglas katika Dakika za 70 na 83 wakati lile la Guangzhou Evergrande lilipachikwa katika Dakika ya 4 na Paulinho.