Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu
24 za makundi A, B, C na D kucheza katika viwanja 12 mbalimbali nchini,
kusaka nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao (StarTime
First League).
Kesho Jumamosi Kundi A, Singida United watakua wenyeji wa Mvuvuma FC
katika uwanja wa Namfua mkoani Singida, Green Warriors watacheza dhidi
ya Mirambo FC uwanja wa Mabatini Mlandizi - Pwani, huku maafande wa
Trasnit Camp wakiwakaribisha Abajalo FC ya Tabora katika uwanja
Kambarage Shinyanga.
Kundi B, jijini Mwanza timu ya Alliance FC itawakaribisha ndugu zao
Pamba FC katika uwanja wa CCM Kirumba, Madini FC ya mkoani Arusha
ikiwakaribisha Bulyanhulu FC uwanja wa Mbulu, huku AFC wakicheza dhidi
ya JKT Rwamkoma katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Kundi C, Abajalo FC ya jijini Dar es salaam watawakaribisha
Changanyikeni FC katika uwanja wa Karume, huku kundi D, Mbeya Warriors
watakua wenyeji wa Wenda FC uwanja wa Sokoine – Mbeya, Sabasaba FC dhidi
ya Mkamba Rangers uwanja wa Jamhuri Morogoro, na The Mighty Elephant
watakuwa wakicheza dhidi ya African Wanderes kwenye uwanja wa Majimaji
mjini Songea.
Jumapili kutakua na mchezo mmoja kati ya Vill Squad dhidi ya
Karikaoo ya Lindi kwenye uwanja wa Karume, Jumatatu Cosmopolitan FC
watawakaribisha Mshikamano FC katika uwanja wa Karume yote ikiwa michezo
ya Kundi C.
No comments:
Post a Comment