Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 19, 2015

GUUS HIDDINK YUPO LONDON KWENYE MAONGEZI NA KLABU YA CHELSEA

Guus Hiddink yupo Jijini London ambako anategemewa kukamilisha mazungumzo ili akalie kiti cha Umeneja wa Chelsea alichotimuliwa Jose Mourinho hapo Jana.
Hiddinck, mwenye Miaka 69, aliwahi kuikaimu nafasi ya Umeneja wa Chelsea Mwaka 2009 na kuiwezesha kutwaa FA CUP.
Mholanzi huyu kwa sasa ni Meneja wa Timu ya Taifa ya Australia na huko tayari wameshatoa ujumbe wa Twitter kwamba ametua Chelsea lakini wakaurekebisha na kudai ni mmoja wa Wagombea wa Nafasi ya Umeneja. Hiddink (katikati kwenye mwaka 2009 baada ya kutwaa Kombe la FA kwenye Uwanja wa Wembley)
Lakini, mmoja wa Wachezaji wa zamani wa Chelsea, Mateja Kezman, amedai Hiddink amepewa wadhifa huo huko Chelsea.
Hii Leo, Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich, alinaswa yuko Cobham, Kituo cha Mazoezi cha Chelsea Jijini London na wengi wametafsiri hilo ni kumkaribisha Hiddink kwa mara ya pili.Kwenye Mazoezi leo hii IjumaaIvanovicKwenye Mazoezi na Mmiliki wa Klabu akiwa karibu na Wachezaji wa KlabuKujiandaa na Sunderland Abramovich akiongea na Kocha/Mwalimu wa Makipa wa Chelsea Christophe LollichonKocha Msaidizi Steve Holland kuiongoza Chelsea jumamosi dhidi ya Sunderland