Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 10, 2015

VAN GAAL ASEMA HANA LA KUJITETEA MAN UNITED KUTUPWA NJE UEFA CHAMPIONS LEAGUE

BOSI wa Manchester United Louis van Gaal amesema hana kisingizio chochote cha kwanini wametolewa kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, na sasa kucheza UEFA EUROPA LIGI.
Hii ni mara ya 4 kwa Man United kushindwa kuvuka hatua ya Makundi ya UCL baada ya Jana kuchapwa 3-2 na Wolfsburg na kushushwa Nafasi ya 3 ya Kundi B na hivyo kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
Licha ya kushindwa kuvuka toka Kundi B ambalo Wachambuzi walihisi kuwa ni jepesi kwani Timu nyingine zilikuwa PSV Eindhoven na CSKA Moscow, Louis van Gaal amesisitiza Man United iko kwenye njia sahihi chini yake.
Alisema: “Kwa sasa siwezi kujitetea lolote kwa sababu tumetupwa nje. Kila neno ntakalosema litakuwa si sahihi. Msimu huu kwenye Capital One Cup tulifika mbali, tulifuzu kuingia Makundi ya UCL na tupo nafasi nzuri kwenye Ligi. Tuko pazuri Zaidi kupita Mwaka Jana