Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akitoa burudani usiku wa kuamkia leo katoka Uwanja wa Lugogo Cricket Oval, Kampala, Uganda.

Diamond akiimba kwa hisia.

Madansa wa Diamond wakiendelea na makamuzi.



Akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
.
USIKU wa
kuamkia leo katika Uwanja wa Cricket wa Lugogo, Uganda, staa wa muziki
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alifunika kwa kupiga
shoo kubwa na ya kihistoria.
Diamond
aliyekuwa ameongoza na madensa wake, muda mwingi aliwakosha mashabiki
hao kwa kuwapigia nyimbo zake zote kali zinazotamba kama vile Kesho,
Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyingine kibao.
Baada ya
kufunika shoo hiyo, Diamond atarejea jijini na moja kwa moja kujiandaa
na shoo nyingine kubwa na ya kihistoria itakayofanyika Sikukuu ya
Krismasi (Desemba 25, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani,
Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Kwa mara ya
kwanza ndani ya Dar Live, Diamond atapiga live kwa kutumia vyombo
nyimbo zake zote kali ikiwa ni pamoja na hii ya Utanipenda ambayo ni
habari ya mjini kwa sasa.
Mbali na
Diamond katika shoo hiyo pia atakuwepo mkali wa nyimbo za Singeli,
Msagasumu ambaye tagonga nyimbo zake zote kali zinazobamba kama vile
Shemeji Unanitega, Huyu Mtoto, Naipenda Simba na nyingine nyingi.
Baada ya
Msagasumu, Mashabiki pia wataburudika na shoo kutoka kwa wakali wa
kucheza nyimbo Afrika Mashariki, Wakali Dancers ambapo watakinukisha
mwanzo mwisho kwa kutoa burudani ya kucheza ngoma zote zinazobamba ndani
na nje ya nchi kwa staili za kipekee.
Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL
No comments:
Post a Comment