Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 26, 2015

JOSE MOURINHO NA DIEGO COSTA WAKWARUZANA KWENYE MECHI

 Jose Mourinho amesema yeye na Diego Costa wameshapatana baada ya kukwaruzana wakati wa Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI, Jana Usiku walipoidunda Maccabi Tel Aviv 4-0 katika Mechi ya Kundi G.
Mourinho hakuridhishwa na kiwango cha Costa katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo.
Meneja huyo alieleza: “Nilisikitishwa,  nikabwata na yeye akajibu. Lakini haftaimu tulikuwa kitu kimoja na kupongezana.”
Bao za Chelsea hiyo Jana zilifungwa na Gary Cahill, Willian, Oscar na Kurt Zouma.
Ushindi huu umeifanya Chelsea wafikishe Pointi 10 sawa na FC Porto ambao Jana walipigwa 2-0 na Dynamo Kiev.
Chelsea na FC Porto zitakutana kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi G Uwanjani Stamford Bridge hapo Desemba 9 na Kikosi cha Mourinho kinahitaji Sare tu ili kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL.
Wakati huo huo, Mourinho ametoboa kuwa nahodha wao John Terry aliumia Enka kwenye Mechi hiyo na Maccabi na yupo hatarini kuikosa Mechi ya Ligi Kuu England Jumapili huko White Hart Lane dhidi ya Tottenham.