MABINGWA wa Ligi Kuu Vodacom, VPL, ambao pia ni Vinara wake, Yanga, wameshinda Ugenini huko Morogoro baada ya kuichapa Mtibwa Sugar Bao 2-0.
Hadi Mapumziko Gemu ilikuwa 0-0.
Kipindi cha Pili Yanga walipiga Bao 2 kupitia Malimi Busungu Dakika ta 53 na Donald Ngoma Dakika ya 89.
Nao Azam FC, wakicheza kwao Chamazi, waliichapa Coastal Union 2-0 kwa Bao za Kipindi cha Pili za Shomari Kapombe na Kipre Tchetche.
Kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Simba iliitungua Stand United Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 58 la Joseph Kimwaga.
Matokeo haya yanaifanya Yanga ibakie kileleni ikiwa na Pointi 15 kwa Mechi 5 sawa na Azam FC lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli na Timu zinazofuatia ni Simba na Mtibwa zote zikiwa na Pointi 12 kila mmoja.
Yanga wavunja mwiko!
Amissi Tambwe anaifungia bao Yanga kipindi cha pili na kufanya 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.Yanga wanapata ushindi wa 2-0 ambao ulichukuwa muda mrefu Tangu 2009
No comments:
Post a Comment