Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 14, 2015

RONALDO AWEKA REKODI KUTWAA BUTI YA DHAHABU ULAYA MARA 4, MWENYEWE ASEMA ANATAMANI TENA ZAIDI

LEO Cristiano Ronaldo ametunukiwa Buti ya Dhahabu ya kwa Ufungaji Bora huko Ulaya na kuweka Rekodi kwa kuitwaa mara 4.
Msimu uliopita, wa 2014/15, Ronaldo alifunga Bao 48 kwenye La Liga na kutwaa Buti ya Dhahabu kwa mara ya 3 akiwa na Real Madrid wakati mara moja alitwaa Msimu wa 2007/08 akiwa na Manchester United.
Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Miaka 47 ya Tuzo hii ya Buti ya Dhahabu kwa Mfungaji Bora wa Ligi za Ulaya kuichukua mara 4.
Mpinzani wa jadi wa Ronaldo, Lionel Messi, ameshika Nafasi ya Pili kwa kufunga Bao 43 katika La Liga Msimu uliopita.
Wakati akikabidhiwa Tuzo yake hii Leo, Ronaldo alisindikizwa na Mama yake, Mtoto wake, Kocha wa Real Madrid, Rafa Benitez, Rais wa Real Florentino Perez na Balozi wa Portugal huko Spain.

Hivi sasa Ronaldo, mwenye Miaka 30, ameifungia Real Jumla ya Mabao 323, sawa na mshika Rekodi wa Bao nyingi katika Historia ya Real, Raul, lakini Jumamosi Staa huyo ana nafasi ya kumpiku Raul wakati Levante ikienda Santiago Bernabeu kuivaa Real kwenye La Liga.

No comments:

Post a Comment