Ligi Daraja la Kwanza nchini (StarTimes First League) inaendelea
wikiendi hii kwa makundi yote matatu kucheza, michezo 11 itachezwa
mwishoni mwa wiki siku za Jumamosi na Jumapili katika viwanja mbalimbali
nchini.
Jumamosi Kundi A, Ashanti United watakua wenyeji wa Mji Mkuu (CDA)
katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, KMC watawakaribisha Polisi
Dodoma katika uwanja wa Mabatini – Mlandizi.
Kundi B, Lipuli FC watawakaribisha Polisi Morogoro katika uwanja wa
Wambi mkoani Iringa, Kimondo FC watakuwa wenyeji wa JKT Mlale kwenye
uwanja wa CCM Vwava – Mbozi, huku Burkinafaso ya Morogoro ikiwakaribisha
Njombe Mji katika uwanja wa Jamhuri.
Kundi C, JKT Kanembwa watakuwa wenyeji wa Panone FC katika uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma, JKT Oljoro watawakaribisha Polisi Moro uwanja wa
Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Geita Gold watacheza na Rhino Rangers
uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita na Polisi Tabora watawakaribsiha Mbao
FC mjini Tabora uwanja wa Ali Hassa Mwinyi.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo miwili ya Kundi A,
Friends Rangers watacheza dhidi ya African Lyon uwanja wa Karume jijini
Dar es salaam, na Polisi Dar watakua wenyeji wa Kiluvya FC katika uwanja
wa Mabatini Mlandizi.
No comments:
Post a Comment