Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 3, 2015

VODACOM YAKABIDHI VIFAA KWA TIMU ZA VPL


Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya mpira wa miguu Tanzania bara leo imekabbidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 490,00,000.
Akikabidhi vifaa hivyo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twisa alsiema kuwa kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakidhi vifaa mbalimbali vy a ligi ambavyo ni jezi za kawaida, jezi za mechi, viatu na vifaa vingine vinayohitajika.

Vijana wakitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini za timu ya African Sport ya Tanga na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 zilizokabidhiwa rasmi leo na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Wanamitindo wakipita kuitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini za timu ya Majimaji na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 zilizokabidhiwa rasmi leo na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, Boniface Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Azam FC pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu ya Azam FC vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, Boniface Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Coastal Union pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Mbeya FC pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Yanga sports club ya jangwani jijini Dar es salaam pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface Wambura na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanamitindo waliokuwa wakizitangaza jezi mpya za timu 16 zitakazoshiriki katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa jezi hizo na vifaa mbalimbali vyenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4.9 na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania kwa timu zote zitakazoshiriki katika ligi hiyo.

“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwaa tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki lii zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya 2015/2016” Alisema Twissa.

Twissa alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata buruddaniya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka sekta hii.

Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiri katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanza ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa” Alisema Twissa.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliishukuru Kampuni ya Vodacom na kuvitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa ligi.

“Ninatoa mwito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa” alisema.

Aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sharia kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya madhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.

Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika mapema pia timu zitakazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.

No comments:

Post a Comment