LEO, katika Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu England huko White Hart Lane, Wenyeji Tottenham Hotspurs waliwachapa Vinara wa Ligi hiyo Manchester City Bao 4-1 na kuhatarisha kupokonywa uongozi wao ikiwa Man United wataifunga Sunderland Leo hii.
City, ambao Wikiendi iliyopita wakiwa kwao Etihad walichapwa 2-1 na West Ham, Leo walitangulia kufunga Bao katika katika Dakika ya 25 kupitia Kevin De Bruyne lakini Eric Dier akaisawazishia Spurs Bao katika Dakika ya 45.
Hapi Mapumziko Spurs 1 City 1.
Kipindi cha Pili, Spurs walicharuka na kupiga Bao 3 kupitia Toby Alderweireld, Harry Kane na Erik Lamela.
3-1Toby Alderweireld 50'Eric Dier anaisawazishia bao Spurs dakika ya 45 na kufanya 1-1 na mpira kwenda mapumziko wakiwa nguvu sawa!1-0BAO la Kevin De Bruyne dakika ya 25VIKOSI:
Tottenham team
wanaonza XI: Lloris; Walker, Alderweireld, Vertonghen, Davies; Alli, Dier; Eriksen, Son, Lamela; Kane
Akiba: Vorm, Rose, Trippier, Carroll, Chadli, Townsend, Clinton
Manchester City team
Wanaoanza XI: Caballero; Sagna, Demichelis, Otamendi, Kolarov; Fernando, Fernandinho; De Bruyne, Sterling, Toure; Aguero
Akiba: Hart, Kompany, Zabaleta, Nasri, Navas, Roberts, Barker
Wachezaji baadhi wa Tottenham wanarejea Uwanjani akiwemo kipa Hugo Lloris, Son Heung-min na pamoja na Dele Alli lakini Vinara wa Ligi hiyo Manchester City hawakumchagua Kipa wao Joe Hart wala Timu Kepteni wao Vincent Kompany kwenye kikosi chao kinachotarajia kuanza dhidi ya Spurs kwenye mehi yao inayotarajia kuanza muda si mrefu.Joe Hart na Vincent Kompany
No comments:
Post a Comment