Mkuu wa mauzo na masoko wa GSM Media, Elibariki Lukumay akizungumza wakati wa mkutano na wandishi wa habari, Kulia ni Katibu wa TASWA, Amir Mhando na Katikati ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto |
KAMPUNI ya GSM Media ya Dar es Salaam imetoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kudhamini tuzo za wanamichezo waliofanya vizuri zaidi katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
Utoaji wa
tuzo hizo utafanyika Oktoba 8, mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam,
ambapo wanamichezo pia watatumia tuzo hizo zilizoandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kumuaga Rais Kikwete
anayemaliza muda wake kikatiba.
Kwa mujibu
wa TASWA licha ya kumuaga Rais Kikwete na kutoa tuzo kwa wanamichezo 10
waliofanya vizuri zaidi, pia chama hicho kitatoa Tuzo ya Heshima Rais Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake
kwa michezo katika utawala wake.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari kutambulisha udhamini huo Dar es Salaam
jana, mwakilishi wa GSM Foundation, Elibariki Lukumay, alisema wameguswa na
tukio hilo na kuona kuna umuhimu wa kuiunga mkono TASWA.
“Taasisi
yetu ambayo ina kampuni mbalimbali imeguswa na kitendo ambacho TASWA inakiandaa
na kwa kuanzia tunatoa kiasi hicho cha fedha kufanikisha jambo hilo na
tunawaomba wengine pia waunge mkono.
“Rais
Kikwete amefanya mambo makubwa katika michezo nchi hii, hivyo tukiwa pia wadau
wakubwa wa michezo tumeona ni vyema tuungane na wenzetu wa TASWA katika kumuaga
na kumshukuru kwa mchango mkubwa alioufanya kwa michezo,” alisema Lukumay.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto aliishukuru taasisi hiyo
na kusema kuwa bajeti ya tukio hilo ni Sh milioni 130 na kwamba wadhamini hao
wamefungua milango kwa wengine ili kulifanikisha jambo hilo.
“Tunaamini
mchango wa Rais Kikwete katika medani ya michezo hauna mfano na kila mdau wa
michezo atakubali amefanya mambo makubwa kwa michezo.
“Tunafahamu Rais alivyosimamia serikali yake kulipia makocha wa michezo ya soka, netiboli na
ngumi. Pia chini ya utawala wake serikali ilipeleka wanariadha wetu China,
Ethiopia na New Zealand kwa maandalizi ya mashindano ya kimataifa,” alisema.
Alifafanua kuwa karibu vyama
vyote vya michezo nchini vitashikirikishwa katika tukio hilo ikiwa ni pamoja
kuwa karibu kwa kila hatua na Wizara Ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
pamoja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
No comments:
Post a Comment